Delivery nchi nzima | Ongea na daktari kwa TSh 10,000 tu

DawaFasta

Kituo cha Afya Yangu

Taarifa za kuaminika kuhusu magonjwa sugu, afya ya uzazi na zaidi - pamoja na huduma za kukusaidia.

Kisukari

Kisukari ni hali ambapo sukari mwilini inakuwa juu kwa muda mrefu. Dalili ni kiu kali, kukojoa mara kwa mara, uchovu na vidonda visivyopona.

  • Pima sukari mara kwa mara nyumbani (glucometer).
  • Kula mlo kamili, punguza sukari na wanga uliokobolewa.
  • Fanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku.
  • Tumia dawa kama ulivyoelekezwa na daktari.

Presha (Shinikizo la Damu)

Presha mara nyingi haina dalili - ndiyo maana huitwa "muuaji wa kimya". Ikidumu inaweza kusababisha kiharusi, matatizo ya moyo na figo.

  • Pima presha angalau mara moja kwa wiki.
  • Punguza chumvi, pombe na sigara.
  • Dhibiti uzito na fanya mazoezi.
  • Usiache dawa bila ushauri wa daktari.

Malaria

Malaria husababishwa na vimelea vinavyoenezwa na mbu. Dalili ni homa, kutetemeka, maumivu ya kichwa na mwili.

  • Pima kwanza (mRDT) kabla ya kutumia dawa.
  • Maliza dozi kamili ya ALu/Coartem.
  • Lala ndani ya chandarua chenye dawa.
  • Mjamzito au mtoto mwenye homa - muone daktari haraka.

Uzazi wa Mpango & Afya ya Uzazi

Chagua njia ya uzazi wa mpango inayokufaa: vidonge, sindano, vipandikizi, kitanzi au kondomu. Kondomu pia hukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa.

  • Ongea na daktari kuchagua njia sahihi.
  • Kidonge cha dharura (P2) kitumike ndani ya saa 72.
  • Pima VVU mara kwa mara - kipimo binafsi kinapatikana.

Upungufu wa Damu

Dalili ni uchovu, kizunguzungu, ngozi kupauka na mapigo ya moyo kwenda haraka. Hutokea sana kwa wajawazito na watoto.

  • Kula mboga za majani, maini, maharage na nyama.
  • Wajawazito watumie Folic Acid na madini ya chuma.
  • Pima FBP (CBC) kujua kiwango cha damu.

Vidonda vya Tumbo

Dalili ni maumivu ya tumbo juu ya kitovu, kiungulia na kujaa gesi. Mara nyingi husababishwa na bakteria H. pylori au matumizi ya dawa za maumivu.

  • Pima H. pylori.
  • Kula kwa wakati, epuka pombe na vyakula vikali.
  • Usitumie dawa za maumivu (NSAIDs) kiholela.

Maelezo haya ni kwa elimu tu na si mbadala wa ushauri wa daktari.

Daktari